Leo Agosti 19, 2017 Serikali imethibitisha na kuwahakikishia Watanzania kuwa ujio wa ndege mpya ya tatu aina ya Bombardier Q400-Dash 8 upo pale pale licha ya baadhi ya wanasiasa wasio wazalendo kutumia kila njia kukwamisha ujio huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Zamaradi Kawawa amesema kuwa kuchelewa kwa ndege hiyo ambayo ilitakiwa kuwasili mwezi Julai mwaka huu kumetokana na majadiliano yanayoendelea ambayo kimsingi yamechangiwa na baadhi ya wanasiasa wasio wazalendo kushiriki kwao moja kwa moja kuweka zuio mpaka pale majadiliano yatakapo kamilika.

“Kuna baadhi ya Watanzania wenzetu wenye maslahi binafsi wanapiga vita ndege hii kuletwa nchini lakini Serikali inawahakikishia wananchi kuwa ndege itakuja na hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi”, alisisitiza Zamaradi.

 

Magazeti ya Tanzania leo Agosti 20, 2017
Video: Vilio, simanzi vyatawala shule ya Lucky Vicent