Vyama vya upinzani nchini vinavyounda Ukawa pamoja na chama cha ACT-Wazalendo, vimeishauri Serikali ya Rais John Magufuli kufuta kazi zote za siasa pamoja na vyama vyote vya siasa nchini kikiwemo CCM.

Akizungumza jana kwa niaba ya vyama hivyo, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa UKAWA, James Mbatia alisema kuwa vyama hivyo vinaishauri Serikali kufanya hivyo ili kuepuka usumbufu wa kuzuia kazi ya siasa ambayo imeanishwa kwenye Katiba.

“Tunamshauri apeleke muswada wa hati ya dharura kwenye Bunge la Kesho kutwa wa kufanya marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wakufutwa vyama vyote vya siasa, tuondoke kwenye siasa ili aongoze anavyotaka yeye,” alisema Mbatia.

Mbatia alikosoa vitendo vinavyofanywa na Jeshi la Polisi kufanya mazoezi barabarani akidai kuwa vinawatia hofu wananchi bila sababu za msingi. Aliongeza kuwa sababu zinazotolewa na Jeshi hilo kuwa wanafanya mazoezi ya kawaida hazina mashiko kwani mazoezi ya aina hiyo hayajawahi kufanyika mitaani tangu Tanzania ipate Uhuru.

Katika hatua nyingine, vyama hivyo vilieleza kukubali wito wa viongozi wa dini nchini wa kurejea Bungeni na kwamba wataanza kushiriki vikao vya Bunge lijalo.

Mbowe afunguka kuhusu kunyang’anywa Jengo la Club Bilicanas
Mwanaume Mmoja Nchini India Abeba Maiti Ya Mkewe Mabegani Kwa Takribani Kilomita 12