Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara amewaomba wasanii wote kutumia wakati vizuri na kuacha kulalamika kutokana na muda wao kuisha bila kuutumia vizuri.

Ameyasema hayo jana jijini Dar es salaam kwenye mkutano kati ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda na wasanii mbalimbali uliokuwa na lengo la kusikiliza kero za wasanii hao.

Aidha, Manara ambaye hivi karibuni alizindua marashi yake siku chache zilizopita, aliwataka wasanii kutolewa sifa bali watumie wakati wao wa umaarufu vizuri kujileteta maendeleo. Alisema endapo hawatautumia muda huo vizuri, watajuta siku za usoni.

”Kuna wasanii wengi wa zamani tuko nao hapa leo, walikuwa maarufu sana kama ninyi mlivyo kwasasa, kuna baadhi waliutumia vizuri umaarufu wao wakafanikiwa, lakini kuna wengine walijisahau wakijua watakuwa maarufu siku zote lakini leo wameporomoka,”alisema Manara.

Msikilize hapa kupata ujumbe wake kwa undani:

Wakuu wa nchi Afrika Mashariki wakutana Arusha leo
Kikosi Maalum cha Polisi chatua mkoani Njombe

Comments

comments