Rais wa TCDB Carolus Bujimu, amesema kuwa wamejipanga ili kutekeleza agizo la Rais Magufuli la kuzitaka Taasisi Binafsi, Mashirika ya umma na Taasisi za Serikali alizoagiza zijipange kwaajiri ya kuhakikisha zinasaidia wasanii wa Tanzania.

Ameyasema hayo mapema hii leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, amesema kuwa wameweka mfumo mzuri katika kuzalisha kazi za wasannii ambapo zitazalishwa kulingana maadili ya kitanzania.

Aidha,Bujimu amesema kuwa wameingia mkataba na Shirika la Posta ambao wao watakuwa wauzaji wa jumla ili kuweza kusukuma mbele gurudumu la Sanaa hapa nchini.

Hata hivyo ameongeza kuwa watafanya kazi na wasanii wa sanaa aina mbalimbali wakiwemo Waimbaji, Waigizaji, Ngoma za Asili na watumia vyombo vya Muziki bila kuwabagua.

Video: Maneno ya Naibu Waziri Anastazia Wambura kuhusu sanaa Tanzania
Mpina awataka wawekezaji kuwa wabunifu katika utunzaji mazingira