Shirika la umoja wa mataifa linalopambana na virusi vya ukimwi (VVU) na ukimwi (Unaids) limesema kundi la vijana wakike nchini wenye umri kati ya miaka 15 na 24 ndio wamekuwa waathirika wakubwa.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mkazi wa shirika hilo hapa nchini Kate Spring wakati wa maadhimisho ya kupambana na ubaguzi na unyanyapaa dhidi ya wanawake na wasichana wanaoishi na virusi vya ukimwi.

Aidha naibu Waziri ofisi ya waziri mkuu anaye shugulikia watu wenye ulemavu, Stella Ikupa amesema jamii inapaswa kuacha ubaguzi kwa watu wenye virusi vya ukimwi huku akibainisha kuwa serikali itazungumza na viongozi wa dini kuweka utaratibu wa kutoa elimu kwa waumini bofya hapa kutazama.

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=X3VY2TIKQ0w]

Bodaboda kutumika kutoa elimu ya Corona
Video: CCM yajuta kumtosa Membe, Mbowe azidi kuwasha moto