Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa upelelezi wa kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji, Akwilina Akwiline umefikia pazuri.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa mpaka sasa upelezi huo unaendelea vizuri.

Amesema kuwa upelelezi huo unafanyika kama kesi zingine za mauaji zilizowahi kutokea, hivyo upelelezi huo ukikamilika jeshi hilo litatoa taarifa.

“Tukio hili nalo tunalifanyia upelelezi ili kujua ni nani alifyatua risasi iliyompiga Akwiline, na sisi tuna wakaribisha Watanzania wote wenye taarifa watuletee kwani milango yetu iko wazi muda wote,”amesema Kamanda Mambosasa

Ngorongoro Heroes yaingia kambini, kujipima dhidi ya Morocco
Ismail Rage: Waarabu wangechezeshwa saa 8:30 au 9:00