Michuano ya kombe la Dunia imeanza rasmi apo jana ambapo wenyeji Urusi wameanza michuano hiyo kwa kishindo baada ya kuichapa Saudi Arabia kwa mabao 5-0 katika mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo uliopigwa kwenye dimba la Luzhniki.

Mabao ya Urusi yalifungwa na Yuri Gazinkiy dakika ya 12, Denis Cheryshev dakika ya 43, Artem Dzyuba aliyepachika bao kwa kichwa dakika ya 71 na dakika za lala salama Denis Cheryshev na Aleksandr Govin wakapachika babao mawili ya haraka.

Hii inakuwa mara ya pili kwa Urusi kutoa kipigo kikubwa katika hitoria ya michuano ya kombe la Dunia ambapo mwaka 1994 Urusi waliichapa timu ya taifa ya Cameroon kwa mabao 6-1.

Tazama video ya magoli yaliyofungwa katika mchezo huo hapa chini;

 

Habari Picha katika swala ya Eid El Fitri viwanja vya Maisara Suleiman mjini Zanzibar
Video: Simulizi saa 70 za muuguzi kutekwa, Ni bajeti ya sekta nyeti

Comments

comments