Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa UVCCM wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) wametoa ufafanuzi kuhusu faida ya ndege mpya zilizonunuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wakisema ndege hizo ni hazina kwa taifa.

Wameyasema hayo jijini Dar es salaam walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari, ambapo wamesema faida kubwa ni kuongeza pato la taifa, na kuiwezesha nchi nchi kufikia uchumi wa kati.

”Kwakweli Ndege hizi Watanzania wanatakiwa wazielewe, kwamba kwanza zitaongeza idadi kubwa ya watalii kwakuwa tu kuna usafiri wenye uhakika na bora zaidi, hivyo kupitia watalii hao uchumi utaongezeka na kuwa imara zaidi,”amesema Howard Shimba msomi wa PHD, UDSM

Mbosso aota kumnunulia Diamond Jumba la Kifahari
Amchinja mwanaye kisa wivu wa mapenzi

Comments

comments