Mwimbaji Vanessa Mdee ameutumia vyema ule msemo wa kigeni kuwa ‘Kisichokuua kinakuimarisha’, na kueleza jinsi ambavyo alivuta pumzi ya mwisho wakati wa misukosuko mizito mwaka huu iliyogeuka kuwa baraka iliyozaa kitu kizito kwenye albam yake mpya ‘The Money Mondays’.

Vee Money ameiambia Dar24 usiku kwenye mahojiano maalum katika hafla ya kusikiliza albam yake mpya kuwa misukosuko aliyoipata ilimfanya ahisi anavuta pumzi ya mwisho na ndipo alipoigeuza biashara kwa kuandika wimbo wa ‘Pumzi ya Mwisho’ na kuwashirikisha Joh Makini na Cassper Nyovest wa Afrika Kusini.

Msikilize hapa akieleza kilichojili:


#OurTake: Dar24 ilipata nafasi ya kusikiliza kipande cha wimbo huo na kama inatoa alama kwa nyota, tunatoa nyota tano za heshima kwa Vee Money.

Hakika hasira za Vanessa kwenye ‘pumzi ya Mwisho’ zilihamia kwenye rap ambayo aliitendea haki iliyowakaribisha Joh Makini na Cassper Nyovest waliofanya mauaji ya haki kwenye ngoma hiyo.

Cassper aka Mr. Full Up ni kati ya wasanii wawili wa juu zaidi Afrika Kusini kwenye ulingo wa muziki wa rap, mwenye heshima kubwa Afrika na duniani kwa ujumla kwa kuvunja rekodi za kujaza kumbi kubwa nchini kwake.

Kwa upande wa Joh anabaki kuwa ‘Makini’ na heshima yake kwa Tanzania imevuka mipaka na sasa ni rapa wa kwanza nchini kwenye muziki wa kizazi kipya kufanya miradi ya muziki mikubwa ya kimataifa, yenye gharama na yenye matunda makubwa.

Unaweza kuweka ‘order’ ya albam hiyo mpya yenye nyimbo rasmi 18 na ziada kwa kubonyeza link kwenye ‘bio’ yake kupitia akaunti yake ya Instagram.

 

TCRA yashusha gharama za kupiga simu
Jux afunguka penzi lake lilivyochangia ‘The Money Mondays’ ya Vanessa