Vanessa Mdee ambaye alikuwa mwanafamilia wa lebo ya B’Hitz iliyowahi kutikisa takribani miaka mitano iliyopita, amesema lebo hiyo ambayo aliachana nayo kwa kutofautiana ilikuwa darasa kubwa kwake.

Mwimbaji huyo aliachana na B’Hitz mwaka 2013 na kuanza safari yake ya muziki kwenye mikono ya uongozi mwingine, huku wimbo wake wa ‘Closer’ ulioandikwa na mdogo wake Hammy B, Amani Joachim ukimpa tuzo ya Kilimanjaro.

Amani na Vanessa hawakuwa kwenye uhusiano mzuri kwa kipindi kirefu kutokana na kutofautiana katika masuala ya kazi.

Hata hivyo, akifunguka katika mahojiano maalum na Dar24, Vee Money amesema kuwa B’Hitz Records inayomilikiwa na mtayarishaji wa muziki, Hammy B ilikuwa ikimfunza mengi na kumtunza kama malkia.

“Nilijifunza vitu vingi sana, they treated me like a princess (walinilea kama binti wa mfalme),” Vanessa alifunguka. “Kuwa kwenye uwepo wao kulinifanya niwe more confident (kujiamini zaidi). Siwezi kusema kuwa walikuwa wananionea bali walinijenga pia and I’m always grateful for that (na ninashukuru kila wakati kwa hilo),” aliongeza.

Katika hatua nyingine, Vanessa amezungumzia wimbo wake wa ‘Kisela’ na namna alivyouandika akijibu swali la Dar24 kama ulimlenga aliyekuwa mpenzi wake, Juma Jux.

Angalia video kupata kiundani majibu ya Vee Money kuhusu jinsi alivyotumia muda wake na Trey Songz jijini Nairobi, mpango wake wa kuanza familia na kuwa na watoto, uhusiano kati ya wasanii wa kike na mengine mengi.

Israel, Palestina kwachafuka, Mahmoud Abbas akata mawasiliano
Magazeti ya Tanzania leo Julai 23, 2017