Vilio vilitawala hii leo katika shule ya msingi Lucky Vicent mara baada ya watoto watatu, Doreen, Wilson na Sadia waliokuwa wakitibiwa nchini Marekani kuwasili shuleni hapo kwaajili ya kuweka mashada kwenye mnara uliojengwa kwaajili ya kumbukumbu ya wanafunzi na waalimu waliofariki katika ajali ya gari.

Watoto hao waliwasili jana kutoka nchini Marekani na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) uliopo mkoani humo.

Video: "Ujio wa Bombardier upo pale pale" - Serikali
Picha: Ziara ya Rais Dkt. Shein Mjini Magharibi, Zanzibar