Viongozi wa dini nchini wametakiwa kuwa mstali wa mbele katika kufanikisha masula ya kimaendeleo ikiwemo ulipaji wa kodi pamoja na kuliombea taifa ili liendelee kuwa na amani na uwajibikaji kwa Watanzania wote.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda alipokuwa akikagua ujenzi wa Ofisi za Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) ambapo amesema kuwa viongozi wa dini bado wana kazi kubwa ya kuhakikisha Watanzania wanakuwa na amani na kuchangia katika ujenzi wa Taifa.

Amesema kutokana umuhimu wa viongozi wa dini, Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano ili kuhakikisha wanafanya kazi ya Mungu katika mazingira rafiki.

“Nafasi ya Mufti ni kubwa sana hivyo tumeona ni vema kupatikana kwa ofisi kubwa ambayo itampa fursa ya kukaa faragha na mungu jambo ambalo ni jema katika kuhakikisha anatoa huduma kwa waumini ya dini ya kislamu katika mazingira bora” amesema Makonda.

Hata hivyo amefafanua kuwa baada ya kukamilika kwa ofisi hizo wataangalia namna ya kupiga hatua zaidi katika kuahakikisha BAKWATA inakuwa na maendeleo.

 

Diva amfukuzia Akon
Video: Uhamiaji yawatoa hofu watumiaji wa 'Passport' za zamani