Kamati ya bunge ya maadili imetangaza kuwasimamisha wabunge wawili wa viti maalum CHADEMA Susan Lymo na Anatropia Theonest kwa makosa ya kulidanganya bunge.

Mbunge Susan Lymo amehukumiwa kwa kusema jeshi la Polisi nchini limenunua magari 777 ya washawasha ikiwa  kwamba hiyo ni idadi ya magari inayopangwa kuingizwa na jeshi hilo kwa ajili ya matumizi mbalimbali.  Kamati imemsimamisha vikao hivyo kuanzia June 17 hadi 24 mwaka huu.

Pia mbunge Anatropia Theonest amesimamishwa kuhudhuria vikao vitatu vya bunge kwa kosa la kulidanganya Bunge kuwa waziri wa ardhi na nyumba William Lukuvi alichukua ardhi ya wananchi akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.

Video: CUF yamtaka Profesa Lipumba asikiyumbishe Chama
TFF Kuzungumza Na DRFA, KIFA