Wabunge wanane waliofukuzwa uanachama na Mwenyekiti anayetambuliwa na Msajili wa Vyama Siasa Nchini wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba leo wametinga mahakamani kupinga uamuzi huo.

Wamefikia hatua hiyo mara baada ya bunge kuridhia taarifa iliyotumwa na Mwenyekiti wa chama hicho kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai ya kuwafukuza uanachama kwa wabunge hao.

Aidha, hivi karibuni Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitangaza majina ya wabunge nane watakaoziba nafasi zilizoachwa wazi na wabunge waliofukuzwa, kitu ambacho kilizua mijadala iliyosababisha hali ya sintofahamu ndani ya chama hicho.

Wolper amtolea chozi Kabula, aomba asaidiwe
Kisa cha muumini kufariki dunia mara baada ya kutoa sadaka