Wachimbaji wadogo wadogo wa madini wameishauri mamlaka ya ukusanyaji mapato nchini (TRA) kupunguza utitiri wa kodi katika sekta ya madini na kuweka mifumo itakayowawezesha wachimbaji hao kuwaondolea kero mbalimbali.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na baadhi ya wachimbaji wadogo wadogo wa madini nchini walipokuwa wakizungumza na Dar24Media, ambapo wamesema kuwa kero kubwa kwasasa ni utitiri wa kodi usiokuwa na mpangilio maalumu

Wamesema kuwa kama TRA ikiweka mazingira mazuri ya ulipaji kodi na kupunguza kodi zisizokuwa za msingi, basi nchi itapata mapato makubwa zaidi kupitia sekta hiyo.

“Niwashauri TRA wakae na sisi wachimbaji wadogo wadogo, tujadili kwa pamoja namna nzuri ya kuweka utaratibu wa kulipa kodi, ni wajibu wetu kisheria lakini mfumo wa ulipaji bado haukizi matakwa,”amesema Magangila mchimbaji mdogo wa makaa ya mawe

Video: Kwa hili nampongeza JPM- Kishimba
Video: NEMC yawageukia wamiliki wa migodi, sasa kukumbana na adhabu kali

Comments

comments