Wafanyabiashara wa mkoani Dodoma wametakiwa  kuboresha biashara zao, kuongeza usafi zaidi na ikiwezekana kuimarisha majengo yao yawe ya kisasa zaidi kwani haiwezekani maduka ya Makao Makuu ya Nchi yawe katika hali isiyovutia.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Oktoba 5, 2016 wakati alipotembelea maduka ya soko la Sabasaba katika barabara ya One Way inayopita katikati ya barabara ya sita hadi ya 11 pamoja na soko la Sabasaba akiwa kwenye ziara ya kukagua maeneo ya kutolea huduma za jamii mjini Dodoma.

Majaliwa ameahidi kukutana na wafanyabiashara hao ili kuzungumzia namna ya kulikarabati na kulifanya liwe la kisasa.

Amesema Serikali tayari imeshahamia Dodoma hivyo wafanyabiashara wanatakiwa kutumia fursa hiyo kwa kuboresha biashara zao ili waweze kumudu ushindani wa soko. Bofya hapa kutazama video

Video: Mzee Chilo ndani ya 'Mtoto mdogo' ya Shilole
Simba Sports Club Kutumia Mgongo Wa Azam FC