Katika kuelekea kuadhimisha miaka 20 ya Kampuni ya DataVision International yenye makao makuu yake Mikocheni Jijini Dar es salaam, wafanyakazi wa Kampuni hiyo wamefuturu pamoja na watoto wenye ugonjwa wa Saratani walioko katika kituo cha Tumaini la Maisha kilichopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Mbali na kufuturu pamoja pia, dataVision wametoa misaada mbali mbali ikiwa ni sehemu ya kuwafariji watoto hao pamoja na kuunga mkono juhudi za kituo hicho kinachofanya jitihada kubwa kuwasaidia watoto wenye ugonjwa wa Saratani nchini.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mfanyakazi wa DataVision Internatinal, MacLeans Mwaijonga amesema kuwa Kampuni hiyo inatimiza miaka 20 hivyo imeunda utaratibu wa kila mwezi ili kuwa pamoja na jamii hasa kwa watu wenye matatizo mbalimbali.

 

Torres na Benitez kuungana tena
Vardy aingia kwenye rada za Atletico Madrid