Moja ya wasanii wakali na mara zote huwa wanafanya kolabo nzuri ndani ya kundi la WCB ni Diamond Platinumz na Rayvany, wawili hao mara zote wakishirikiana kufanya kazi ya muziki huwa ni moja ya nyimbo kali zinazopendwa na kutazamwa zaidi na watu mbalimbali.

Sasa baada ya Salome wakaja na Iyena ikafuta Nyegezi sasa ni zamu nyingine tena ambapo wamedondosha moja ya nyimbo kali na iliyopendwa zaidi kuanzia Audio mpaka Video inayoenda kwa jina la “Tetema’.’

Na moja ya shairi limeimbwa na Bosi wa WCB, Diamond Platinumz anasema ‘Tetema kama umepigwa ngeta’ ni moja ya mstari ninaoukubali zaidi.

Tetema ni moja ya nyimbo kali kwani mara baada ya kuachiwa ndani ya masaa machache imetazamwa na watu zaidi ya Milioni moja, rekodi ambayo imewahi kuvunjwa na mpinzani wake Alikiba miaka michache iliyopita na nyimbo yake ya Seduce Me.

Tazama hapa video yote, Dar 24 imekuwekea karibu.

WCB ni lebo kubwa hapa Afrika Mashariki iliyojikita na kusajili wasanii chipukizi na wenye viwango vya kufanya muziki mzuri kama ambavyo wanafanya.

Na Diamond ni msanii mzuri anayefanya muziki mzuri na unaokubalika na watu wengi zaidi ndani na nje ya nchi, na hii imedhihirika kutokana na shoo kali na nyingi anazokuwa anazifanye nje ya Tanzania lakini pia ndiye msanii pekee anayeongoza kwa kufanya kolabo na wasanii wakubwa hapa duniani akiwemo  Rick Ross, Omario, Ne-yo na wengine wengi hapa barani Afrika.

Watangazaji wa Kenya na Wakenya kwa ujumla bado wanautukuza ujuzi wa Diamond katika muziki na kujaribu kuuliza na kufananisha kwa sasa ni msanii gani nchini kwao anayeweza kufanya nyimbo kali na kubwa itayotazamwa ndani ya masaa machache na kufikisha idadi hiyo ya watazamaji.

 

 

 

Video: DC Mtwara aonya upotoshaji wa taarifa dhidi ya mauzo ya Korosho
Janga la Mimba Mashuleni laukumba Mkoa wa Kigoma

Comments

comments