Wakili wa Kujitegemea nchini, Leonard Manyama amemtaka mbunge wa Singida Masharika kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu kujitafakari aina ya maisha aliyoamua kuishi ya kuichafua Tanzania kimataifa.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa ni kosa kubwa kuichafua nchi.

Amesema kuwa Lissu yuko barani Ulaya kwaajili ya matibabu lakini cha ajabu ameamua kufanya ziara ya kuichafua nchi kupitia mgongo wa matibabu.

“Lazima mjiulize ni nani anayemdhamini Lissu katika ziara zake za huko Ulaya, Matamshi anayoyatoa dhidi ya taifa letu, huku yeye akijiita mzalendo, yanalijenga au yanabomoa taifa? Tundu Lissu ni lazima ajitathimini maisha aliyoamua kuishi,”amesema Manyama

Aidha, siku za hivi karibuni, Mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amekuwa akifanya ziara barani Ulaya huku akizungumzia masuala mbalimbali ya nchi.

 

Wananchi waishio mipakani watakiwa kuchangamkia fursa
Waganga wa Jadi wawekwa kitimoto mkoani Njombe

Comments

comments