Wakili wa Kujitegemea nchini, Leonard Manyama amesema kuwa muswada wa sheria ya vyama vya siasa ni mzuri, hivyo wanasiasa wanatakiwa kujumuika kutoa maoni yao ili uweze kutoa dira nzuri ya demokrasia.

Ameyasema hayo jijijni Dar es salaam mara baada ya kumalizika kwa Kongamano la siasa lililoandaliwa na chama cha mapinduzi (CCM), ambapo amesema ni vyema wanasiasa wakashiriki wote ili kuweza kubaini vifungu ambavyo havistahili kuwepo kwenye muswada huo ili viondolewe.

”Kwakweli kwa upande wangu nauona muswada huu uko sahihi, ingawa kuna baadhi ya vifungu vichache vya kufanyiwa marekebisho, hivyo basi nawasihi wanasiasa wasiukimbie muswada huu, wajumuike kwa pamoja watoe maoni yao ili uweze kurekebishwa kwenye mapungufu,”amesema Manyama

Video: Polepole afunguka kuhusu Msajili wa Vyama vya Siasa, 'Amekuwa Mungu mtu'
Mahakama yakataa kupokea kesi kuhusu CAG na Spika, Jaji Mkuu aandika barua

Comments

comments