Wakulima wa kilimo cha Mpunga katika skimu ya kilimo cha Umwagiliji ya Dakawa wamenufaika na kilimo hicho baada ya serikali kukarabati mindombinu ya umwagilijai ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara, ofisi, ukarabati wa pump na mifereji ya upili.

Hayo yameelezwa Mjini Dakawa na Mhandisi wa Kanda ya Morogoro kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Senzie Meeda alipozungumza na waandishi wa habari walipotembelea skimu ya umwagiliaji ya Dakawa.

Mhandisi Meeda ameeleza kuwa Serikali kupitia shirika la kimaitaifa la misaada la Marekani USAID imetumia takribani kiasi cha shilingi Bilioni 20, katika ujenzi wa skimu hiyo,  na mpaka sasa asilimia themanini (80%) ya kazi hiyo inaendelea vizuri na inategemea kukamilika mwezi December mwaka huu.

“Njia zote za kwenda mashambani zinapitika, maeneo ya pembezoni ambayo yalikuwa hayafikiki mwanzoni sasa yanafikika, Pump Mpya za kisasa zinazotumia umeme mdogo zimefungwa hivyo uzalishaji umeongezeka ambapo mkulima anaweza kuvuna hadi tani sita (6) kwa hekta hili limesaidia sana kuongeza kipato na kutengeneza ajira.” Amesema Mhandisi Meeda.
Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa chama cha wakulima wadogo wa umwagiliaji Dakawa, Bertha Chilosa, ametoa shukrani kwa serikali kwa niaba ya wakulima wa dakawa na kusema kuwa kilimo kimekuwa na uchumi mkubwa katika eneo hilo na kubadilisha maisha yao na kuiomba serikali kuwasaidia wakulima hao kutafuta masoko ya uhakika ili kuwe na bei ya uhakika.
“Naiomba serikali itusaidie katika jambo hili, maana kutokuwa na soko la uhakika kunasababisha madalali wanakuja hapa kununua mpunga kwa bei ya kulangua na kutasababishia sisi wakulima wadogo kupata hasara, Naiomba serikali ichukue jukumu hili, ili mkulima asinyanyasike, sambamba na hili, ninaiomba serikali iongee na Mabenki ili yaweze kutupunguzia riba katika mikopo tunayopewa.” Ameisisitiza Bertha

 

Video: Manny Pacquiao ampiga Matthysse kwa KO
Makonda aeleza mafanikio ya Serikali katika mkoa wa Dar es salaam