Wakili wa Kujitegemea, Leonard Manyama amesema kuwa Wakurugenzi wana haki ya kusimamia uchaguzi kwani wakishateuliwa kuwa wakurugenzi hawaruhusiwa kuendelea na itikadi za vyama vyao.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa kuna watu wanaeneza propaganda kuhusu wakurugenzi kusimamia uchaguzi mkuu.

Amesema kuwa wakurugenzi hao huwa wanasimamia uchaguzi kwa mujibu wa sheria na si kama baadhi ya wanaharakati wanavyoeneza propaganda katika mitandao mbalimbali ya kijamii kwa maslahi yao binafsi.

Aidha, amesema kuwa kuna watu wanatafasiri vibaya Ibara za katiba na kueneza upotoshaji mkubwa kuhusu wakurugenzi, hivyo ameawataka wananchi na jamii kwa ujumla kuzipuuza propaganda hizo.

”Mimi niseme kwamba hapa sheria na vifungu vya katiba vimetafasiriwa vibaya kwaajili ya kutaka kuipotosha jamii na watu wenye maslahi yao binafsi wanayoyajua,”amesema Manyama

Mwalimu kuburuzwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa
Iran yazitaka China na Urusi kuulinda mkataba wa Nyuklia

Comments

comments