Shule za Umma zimeonekana kutofanya vizuri katika matokeo ya Mitihani mbalimbali ya shule za misingi na sekondari ikilinganishwa na zile zinazomilikiwa na watu binafsi au taasisi zisizokuwa za Kiserikali.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Ubunifu Tanzania, (EIT), Benjamin Nkonya alipokuwa akizungumza na Dar24 Media ambapo amesema kuwa Walimu wabovu na usimamizi mbaya uliokuwepo hapo awali ndio chanzo cha matokeo hayo mabovu.

Amesema kuwa kuna changamoto nyingi ambazo zinazikabiri shule za Umma ambazo kama jamii ikiungana zinaweza kutatuliwa kirahisi zaidi.

“Unajua hapo awali hapakuwa na mfumo mzuri wa usimamizi wa elimu katika shule za umma, Walimu walikuwa wakijiamlia cha kufanya, lakini kwasasa limethibitiwa na serikali ya awamu ya tano, tunashukuru kwa hilo,”amesema Nkonya

Video: Gwajima ampongeza JPM, 'Leo umekuwa Nabii'
Video: Makonda amchongea Tundu Lissu kwa JPM, 'Akirudi apelekwe Milembe'