Taasisi ya elimu ya watu wazima Mkoani Kagera imewataka walimu kujiendeleza kimasomo ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi na kuingia katika ushindani wa ajira sambamba na kuinua kipato chao ambapo wakishajiendeleza maslahi yao yataboreshwa.

Akizungumza katika semina ya kuwahamasisha walimu wa manispaa ya Bukoba Mkoani kagera iliyofanyika shule ya msingi Tumani julai 30 mwaka huu, Mkufunzi Mkazi kutoka taasisi ya elimu ya watu wazima Mkoa wa Kagera, Josefine Rwechungula amewataka walimu hao kulipa kipaumbele suala la kujienedeleza kimasomo bila kujali umri wao maana elimu haina mwisho.

“Tunatarajia kufungua kituo cha kutolea elimu ya watu wazima na elimu masafa mnamo mwezi disemba mwaka huu ili kuweza kutoa fursa kwa walimu kujiendeleza kielimu huku wakiwa katika maeneo yao ya kazi, ninachoshukuru mwitikio ni mzuri walimu wanajitokeza kwa wingi tulianzia Missenyi hamasa ilikuwa kubwa na tayari wameshaanza kujisajiri.” amesema .Josefine

Kwaupande wake afisa elimu taaluma Mkoa Kagera, Mbaraka Maya amesema kuwa walimu ama watumishi wanapo jiendeleza zipo faida mbili mbazo zinatokana na mtu aliyejiendeleza kielimu na huduma ikaonekana kwa wananchi.

“Mtumishi anapojiendeleza faida zipo nyingi ila kubwa zaidi ni mbili, kwanza ni kwa serikali pale mtumishi  aliyejiendeleza anatoa huduma iliyo bora kwa wannachi na kuifanya serikali kupata sifa kwa ubora wa huduma ya mtumishi, lakini nyingine ni kwa mtumishi mwenyewe akishajiendeleza anaongeza kiapto chake na levo ya mshara pamoja na cheo” Amesema Mwl.Maya.

Hata hivyo, zaidi ya walimu 190 kutoka katika shule za msingi za serikali ndani ya manispaa ya Bukoba wamejitokeza katika semina hiyo ambapo wameonyesha kuvutiwa na suala la kujiendeleza.

Watanzania tunaweza, tunachotakiwa ni kujiamini- Rais Magufuli
Magufuli amtengua DED Halmashauri ya Wilaya Morogoro