Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage kuwanyang’anya wote walioshindwa kuendeleza viwanda vyao.

Ametoa agizo hilo mapema hii leo mkoani Tanga katika uzinduzi wa Kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro kilichopo mkoani humo, amesema kuwa hakuna sababu yoyote ya kuwa mtu anayemiliki kiwanda wakati amesindwa kukiendeleza.

“Hakuna maana yeyote ya kuwa na mtu ambaye anamiliki kiwanda, halafu hakiendelezi, nakuagiza wanyang’anye bila kujali cheo chake, hata kama ni waziri, au mtangulizi wako nyang’anya, mimi ndiye Rais hakuna wa kukutisha,”amesema Rais Dkt. Magufuli

Aidha, katika hatua nyingine amempongeza mwekezaji wa Kiwanda hicho kwa kuweza kudharisha ajira zaidi ya mia tatu, hivyo kuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa eneo husika.

Hata hivyo, Rais Dkt. Magufuli amemtaka Waziri Mwijage kutokuwa na kigugumizi katika maamuzi anayoona ni sahihi, kwani viwanda hivyo ni mali ya Watanzania na si wawekezaji.

Mwijage awataka wamiliki wa viwanda kujisalimisha
Wenye Magari yenye 'tinted' Dar kukiona cha moto