Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambulika na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba amesema kuwa waliozuia mkutano wa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif mkoani Mtwara ni viongozi wa Wilaya kwani amepanga kufanya mkutano huo kinyume na utaratibu hivyo viongozi hao waliwapigia simu Jeshi la Polisi kuzuia mkutano huo.

Prof. Lipumba amesema hayo leo Novemba 23, 2016 wakati akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za Chama hicho zilizopo Buguruni jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa kati ya mambo yaliyopelekea Wanachama wa CUF Mtwara kuzuia mkutano wa Maalim ni ajenda yake mbovu ya kutaka kumfukuza uanachama Mbunge wa Mtwara mjini, Maftaah Nachuma ambaye amechaguliwa na wananchi. Tazama hapa

Mzee Mwinyi akiri Magufuli ‘amefunika’ kazi ya watangulizi wake
Makonda: Sitaki watumishi mizigo katika mkoa wangu