Maelfu ya waandamanaji wanaompinga mgombea anaewania nafasi ya kupeperusha bendera ya Republican kwenye uchaguzi wa Rais wa Marekani, Donald Trump wakitumia wimbo wa Kendrick Lamar ‘Alright’.

Waandamanaji wanaompinga Donald Trump

Waandamanaji wanaompinga Donald Trump

‘Alright’ ni wimbo wa rapa huyo ulioko kwenye album yake ya mwaka jana, To Pimp A Butterfly iliyong’ara kwenye tuzo za Grammy na kuendelea kumhakikishia rapa huyo kuwa yeye ndiye rapa bora zaidi wa kizazi hiki. Huu ni wimbo wa kutia matumaini kwa walio mashakani.

Ijumaa iliyopita, muda mfupi baada ya kutokea vurugu kubwa kwenye mkutano wa kampeni wa Trump huko Chicago uliolazimika kuahirishwa, mamia kwa maelfu ya waandamanaji walifurika mitaani wakionesha mabango yenye jumbe mbalimbali za kumpinga mwanasiasa huyo huku wakiimba kiitikio cha wimbo huo.

Hii sio mara ya kwanza kwa waandamani kutumia wimbo huo kujipa matumaini wakati wakidai au kupinga jambo fulani. Julai mwaka jana, wanaharakati waliokuwa wanapinga kukamatwa kwa kijana mweusi mwenye umri wa miaka 14, walitumia wimbo huo wakati wakiandamana.

Januari mwaka huu, Meya wa Jiji la Compton alitangaza kumkabidhi Kendrick Lamar ufunguo wa jiji hilo kutokana na mchango wake. Kadhalika, Rais wa Marekani, Barack Obama alimkaribisha rapa huyo Ikulu baada ya kuvutiwa na wimbo wake wa ‘How Much a Dollar Cost’.

Zlatan Atangaza Msimamo Mkali Wa Kubaki Jijini Paris
Rais wa Malawi apinga utabiri wa T.B Joshua kuhusi kifo chake, amuita Muongo