waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Maofisa Elimu nchini kufanye ukaguzi katika shule ili kubaini wanafunzi hewa kwenye mpango wa elimu bure.

Majaliwa amesema kila mwezi Serikali inapeleka shule zaidi ya shilingi bilioni 18 kugharamia elimu bure na sasa umeanza kujitokeza udanganyifu katika sekta ya elimu kwa kuwa na wanafunzi hewa.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana alipokutana na watumishi na viongozi wa Manispaa ya Ilala katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

 

 

Diego Simeone: Sikuwahi Kusema Hadharani Ninataka Kuondoka
Lema afunguka uteuzi wa Mkuu wa Mkoa Mpya Arusha, "Nilijua..."