Wanaharakati kutoka taasisi mbalimbali za kutetea haki za binadamu wamesema kuwa wanakusudia kwenda mahakamani kufungua kesi ya kupinga Wakurugenzi wa Halmashauri ya miji na majiji kusimami shughuli mbalimbali za uchaguzi.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na wakili wa kujitegemea kutoka Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema kuwa haiwezekani wateule wa rais wakasimamia chaguzi mbalimbali hapa nchini kwani kuna uwezekano mkubwa wa kupendelea upande mmoja.

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Februari 28, 2018
Emmanuel Okwi kuivaa Stand United