Wananchi wameshauriwa kuwa na tabia ya kupima afya mara kwa mara ili kuweza kuepukana na magonjwa mbalimbali kama vile kifua kikuu.

Hayo yamesemwa na Isack Lekule Msaidizi wa Mratibu wa Kifua Kikuu Sugu kutoka Wizara ya Afya, alipokuwa akizungumza na Dar24 Media ambapo amesema kuwa kuna aina mbili za ugonjwa wa kifua kikuu ambazo ni Kifua Kikuu Sugu na Kifua Kikuu cha kawaida.

Amesema kuwa mgonjwa wa Kifua Kikuu cha kawaida hutibiwa na kupona ndani ya miezi sita, lakini Kifua Kikuu Sugu hutibiwa ndani ya miezi kumi na mbili.

“Wagonjwa wa kifua kikuu hutibiwa na kupona, lakini hutofautiana muda wa kupona kulingana na mgonjwa mwenyewe, kifua kikuu cha kawaida hupona ndani ya miezi sita, lakini kifua kikuu sugu hupona ndani ya miezi nane hadi kumi na mbili,”amesema Lekule

Mbeya City kuwavaa Simba bila Hassan Mwasapili, John Kabanda
Singida Utd watamba kuivurugia Young Africans

Comments

comments