Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewataka wanao hoji fedha za serikali zinakwenda wapi wamfuate yeye au wafike ofisini kwake ili aweze kuwaonyesha fedha hizo zinapokwenda na kuwaonyesha miradi inayofanywa na serikali ya awamu ya tano.

Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam wakati akieleza mpango wa ujenzi wa miradi mbalimbali Jijini humo, ikiwepo stendi ya kisasa ya Basi ambayo inakusudiwa kujengwa Mbezi Luis pamoja na ujenzi wa Machinjio ya kisasa na kusema kuwa hiyo miradi ndiyo itakayomrudisha Rais Magufuli vizuri katika uchaguzi wa mwaka 2020.

“Nasema kama kuna mtu anataka kujua fedha za serikali zinakwenda wapi kama huko kwingine kote haoni basi aje Dar es Salaam mimi Makonda nitamuonyesha fedha zinakwenda wapi. Tuna bilioni zaidi ya 700 zinazokwenda kutusaidia sisi kujenga barabara, mifereji na kubadilisha jiji letu na ukipita sasa hivi utaona hata lami inayojengwa sasa ni tofauti na miaka mingine,”amesema Makonda

asema kama kuna mtu anataka kujua fedha za serikali zinakwenda wapi kama huko kwingine kote haoni basi aje Dar es Salaam mimi Makonda nitamuonyesha fedha zinakwenda wapi. Tuna bilioni zaidi ya 700 zinazokwenda kutusaidia sisi kujenga barabara, mifereji na kubadilisha jiji letu na ukipita sasa hivi utaona hata lami inayojengwa sasa ni tofauti na miaka mingine,”amesema Makonda

Magazeti ya Tanzania leo Mei 11, 2018
Yanga yachezea kichapo, yakabidhi kombe Msimbazi

Comments

comments