Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewataka wasanii kuwa wazi pindi wanapopata fursa ya kukutana na viongozi mbalimbali wa serikali.

Aliyasema hayo jana jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wake na wasanii mbalimbali ambapo amewataka kuacha tabia ya kuficha mambo yanayowakabili wakikwepa kuonekana hadharani.

Amesema kuwa hakuna mtu asiyejua kuwa wasanii kwasasa hali zao si nzuri, hivyo amewataka kujiwekea mikakati ambayo inaweza ikawasaidia na kuwawezesha kupata mkopo katika taasisi mbalimbali yakiwemo mafungu ya hela za vijana yanayotolewa serikali.

”Unajua unapopata nafasi ya kukutana na kiongozi wa ngazi za juu wa serikali ni lazima uitumie hiyo fursa, jengeni tabia ya kuwa wawazi, hakuna asiyejua kuwa nyie mmefulia, nasema hivyo kwasababu nawafahamu vizuri,”amesema Makonda

Makonda aliitisha mkutano na wasanii mbalimbali kwa ajili ya kusikiliza kero zinazowakabili, na kuangalia namna atakavyoweza kuwasaidia kukuza sanaa zao.

Marekani yaishushia makombora Al-Shabaab
Wakuu wa nchi Afrika Mashariki wakutana Arusha leo

Comments

comments