Msanii wa hip hop nchini anayetamba  kwa wimbo wake wa ‘KAMA UTANIPENDA’ Ramadhan Sharrif Maarufu (Darasa) ametangaza wimbo wake mpya unaoitwa ‘TOO MUCH’ wimbo huo mpya umerekodiwa kupitia studio ya Mr.T Touch.  Pia Darasa alitumia nafasi hiyo kutambulisha lebo yake rasmi  ya Classic Music Group(CMG) ambayo itakua inafanya kazi kwa misingi ya kuinua vipaji vya chipukizi watakaoonyesha uwezo katika muziki wa hip hop.

Mwana Hip hop huyo alieleza kuaminika na watu hasa wasanii wenzake aidha kwa kazi zake nzuri au life style yake.

“Kila iitwayo leo katika kazi zangu nikiifanya bora zaidi ya jana nashukuru watanzania wamenielewa kazi zangu, sasa leo niwaletea kitu kipya cha ‘Too Much’ ambacho nimefanyia hapa bongo, nimefanikiwa kuufanya muziki wangu kuwa wa tofauti katika ladhaa zake, mtihani wangu ndiyo huu kwa shabiki” – Darasa

Lebo Za Kusimamia Kazi za wasanii Zinakuza Mziki wa Bongo?
Pesa zamlaza hospitalini Rita Ora