Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amewataka wananchi kutokubali kurubuniwa kuandamana na watu waliopo nje ya nchi maana watakumbana na mkono wa sheria.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Dar24 Media ambapo amewataka wananchi kuwapuuza watu ambao wamekuwa wakihamasisha maandamano mitandaoni.

Amesema kuwa maandamano yana utaratibu wake hivyo ni bora kuomba kibari ili waweze kupatiwa ulinzi na si vinginevyo.

“Maandamano yana utaratibu wake, na nawaomba wananchi wawapuuze hao wanaohamasisha maandamano kwenye mitandao wakati wao wako nje ya nchi, watawasababishia matatizo bure kwasababu watakumbana na mkono wa sheria,”amesema Kamanda Mambosasa

Makonda kuwanyoosha wanaume wa Dar wanaokimbia mimba zao
Tillerson atofautiana msimsmo na Trump kuhusu Afrika