Taasisi ya Tumaini la Maisha inayosaidia watoto wenye saratani wanaopata matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, imelenga kuhakikisha inawafikia na kuwapa msaada wa kitabibu watoto wote wenye saratani nchini kwa kushirikiana na wadau wake.

Akizungumza na Dar24 kwenye mahojiano maalum, Mkurugenzi wa Misaada wa Taasisi hiyo, Alex  Kaijage ameeleza jinsi ambavyo taasisi hiyo imepiga hatua tangu mwaka 2011 pamoja na hali halisi ya watoto wanaopata saratani nchini.

Kaijage ambaye ametaja hospitali ziliko ndani na nje ya mkoa wa Dar es Salaam wanazoshirikiana nazo, amesema kuwa pamoja na changamoto zinazowakabili, wanatarajia kupata kesi mpya za watoto wenye saratani kati ya 3,000 hadi 4,000 kwa mwaka na ameeleza jinsi walivyojipanga.
Angalia hapa mahojiano yote:

 

 

Bi Sandra aigomea harusi ya Diamond na Hamisa
Nandy afuata nyayo za Diamond, Alikiba