Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete amechangia ujenzi wa vyoo viwili vya kisasa katika jimbo la Chalinze huku kimoja akijenga Bagamoyo.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Dar24 Media jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kuchangia kampeni ya ujenzi wa vyoo katika shule mbalimbali za watoto wa kike nchini iliyoandaliwa na wabunge wanawake.

“Unajua sisi wabunge wa kiume tumeguswa sana na wabunge wanawake, ndio maana tumeamua kuunga mkono kampeni hii, kwa hiyo kufanya hivi tunawasaidia watoto wa kike ili waweze kutimiza ndoto zao, mimi binafsi nimechangia kujenga vyoo viwili ambapo kimoja kitakuwa Chalinze na kingine Bagamoyo,”amesema Ridhiwani

 

 

Video: Nape amchana Prof. Jay, asema hana jipya
Mnada wa Makontena ya Makonda Wafana Jijini Dar

Comments

comments