Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa amesema kumekuwa na magonjwa yasiyopewa kipaumbele na yameathiri sehemu kubwa ya jamii katika Mkoa wa Dar es salaam na kuleta mahangaiko kwa wananchi hali ambayo inapunguza uwezo wa wananchi kushiriki katika shughuli mbali mbali za ujenzi wa Taifa.

Mgandilwa amesema hali hiyo pia imesababisha watoto kutoweza kuhudhuria vizuri katika masomo ya shuleni.

Amesema magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, pamoja na kusababisha usumbufu mkubwa kwa waathirika wa magonjwa hayo, pia yanaongeza matumizi ya rasilimali chache zilizopo katika kuyakabili magonjwa haya.

Amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na wadau wamekuwa wakitoa dawa za kutibu na kukinga magonjwa hayo katika nchi nzima.

Kufuatia juhusdi hizo za Serikali kupitia mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ulioanzishwa mwaka 2009, umeweka kambi katika Zahanati ya Pugu ya Manispaa ya Ilala kwa ajili ya kutoa tiba kwa magonjwa yasiyopewa kipaumbele na itaanza na kufanya upasuaji kwa watu wenye tatizo la mabusha ambapo watu wapatao 400 watapatiwa huduma hiyo na hakuna malipo.

Huduma hiyo imetajwa kuendelea katika  kwenye manispaa nyingine hapo baadae.

Aidha, Serikali itagawa dawa za kingatiba kwa jamii yote inayoishi katika mkoa wa Dar es salaam ambapo zoezi hilo linatarajiwa kufanyika mwezi huu wa kumi(10) kuanzia tarehe 25 hadi tarehe 29 2016, zoezi hilo likihusisha watu wote wenye umri kuanzia miaka mitano(5) na kuendelea ambapo watameza dawa za Mectizan na Albendazole za kukinga na kutibu magonjwa ya minyoo na tumbo, matende na mabusha katika manispaa zote za mkoa wa Dar es salaam.

Video: Mfalme wa Morocco kujenga uwanja wa mpira Dodoma utakaogharimu dola milioni 100.
Video: Ali Kiba aeleza kwanini hajikiti kusaka collabo za kimataifa