Kufuatia kutangazwa kwa Donald Trump kuwa Rais mteule wa Marekani, wananchi wa Marekani wameandamana katika miji saba kupinga ushindi huo wa Trump.

Waandamanaji hao wamekusanyika nje ya mnara maarufu wa Trump ‘ Trump Tower’  mjini New York wakipaza sauti za kumpinga Trump. Wengine walionekana nje ya Ikulu ya Marekani wakipaza sauti kuwa “Not my president” (Si Rais wangu), pamoja na mabango mengine.

Wengi wa waandamanaji walioongea na CNN wameelezea kuwa wana wasiwasi sana kuhusu Trump kwavile kuongoza Marekani sio kama kuiongoza nchi yoyote duniani.

“Kwa matokeo haya tumeiangusha Dunia. Trump hakustahili kuwa Rais. Nahisi watu walipiga kura kwa hasira lakini Trump ni hatari kwa dunia,” alisema mmoja wa waandamanaji aliyejitambulisha kwa jina la James Betwell kutoka Califonia.

Cristiano Ronaldo Atafuta Hifadhi Sporting Lisbon
Video: Obama amkaribisha Trump 'White House'