Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya imesema kuwa imebaini mtandao wa watumiaji na wauzaji ambao umekuwa ukijihusisha kwa siku nyingi.

Hayo yamesemwa mjini Dodoma na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kuzuia Dawa za Kulevya, Rogers Sianga, ambapo amesema baada ya kuugundua mtandao huo kazi inayofuata ni kuwashughulikia.

Amesema kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara Watanzania waliomo katika mtandao huo wamekimbili nchi jirani huku wakiendelea kufanya biashara hiyo wakiwa huko.

“Kinachofuata kwa sasa ni kuwashughulikia kwasababu tayari tumeshaubaini mtandao mzima, hivyo tunatumia njia zetu ili tuweze kuwakamata walioko nje ya nchi ili tuwajumuishe na hawa waliopo nchini,”amesema Sianga

Vita ya dawa za kulevya yamponza Durtete
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Februari 9, 2018