Wazazi na walezi wenye watoto wanaosoma wameonywa kuhujumu ndoto za watoto kwa kuwashawishi kufanya vibaya katika mitihani yao ya mwisho kwa lengo la kuwafanya watoto hao kutoendelea na masomo yao ya baadae na badala yake kuwatumia katika mambo yao ikiwemo kuwaozesha na wengine kuwafanyisha kazi za kilimo na ufugaji.

Onyo hilo limetolewa na mdau wa maendeleo na mkurugenzi wa kampuni za Boma Security Company Ltd, Evance Kamenge  alipokuwa akiwahutubia wazazi,walezi, walimu pamoja na wanafunzi kwenye mahafari ya darasa la saba katika shule ya msingi Nyabihanga iliyopo  wilayani Missenyi mkoani Kagera.

“Serikali inatoa pesa nyingi kuwasomesha watoto wenu na pesa hizo zinatolewa Zaidi ya shilingi bilioni 23 kila mwezi za elimu bure, cha ajabu wapo wazazi na walezi wachache wenye malengo mabaya na kuwashawishi watoto wao kufanya vizuri kwenye mitihani yao ili wasifahulu, mimi niseme tu kwa mzazi yeyote atakayebainika nitachukua jukumu la kumshitaki katika vyombo vya sharia kwa hujuma hizo.” Amesema Kamenge.

Zaidi ya wanafunzi 610 katika kata ya Kasambya wilayani Missenyi wamefanya mtihani wa darasa la saba, wanafunzi 585 wamefahulu mtihani huo katika matokeo yaliyotangazwa siku chache zilizopita ambapo wazazi wametakiwa kujiandaa ili kuhakikisha watoto hao wanakwenda sekondari,…Bofya Hapa kutazama.

Video: MAJONZI! kijana aliyepumlia Mashine, alikisema kifo chake, Neno lake la mwisho lawaliza ndugu
Mwenyekiti Chadema akamatwa kwa kupandisha bendera barabarani