Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema katika jitihada za Serikali kupambana na kuzuia watu wasipate vifo vinavyotokana na Saratani ya mlango wa kizazi imeongeza huduma za kupima na matibabu ya awali ya ugonjwa huo katika mikoa 10, ambapo katika mikoa hiyo zitachaguliwa Halmashauri tatu na kila Halmashauri vitawekwa vituo vitatu.

Aidha, Waziri Ummy amesema huduma za chanjo zitaanza kutolewa kwa wasichana wa miaka 9 – 13 hivyo amewatoa wananchi wasiwasi kuhusu huduma hizo kwani hata yeye atakuwa wa kwanza kumtoa mtoto wake ili apatiwe chanjo hiyo ya kujikinga na maambukizi ya Saratani ya shingo ya uzazi.

TRA yapata tuzo ya utunzaji wa hesabu za taasisi za umma
DC akanusha kulala chooni na familia yake, asema hatishiki