Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene ameitaja mikoa ambayo imetimiza na kukamilisha mpango wa madawati ambao utasaidia kuondokana na tatizo la wanafunzi kukaa chini

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam, aidha amesema pamoja na kukamilisha kwa kuvuka malengo hayo amewataka amewataka wakuu wa mikoa hiyo, kuweka uwiano na mpangilio mzuri wa mgawanyo ili shule zote ziweze kupata madawati .

Aidha, katika hatua nyingine, Simbachawene ameitaja mikoa mingine ambayo haijfikia lengo na bado ina upungufu mkubwa wa madawati,na kutoa wito kwa wakuu wa mikoa hiyo, wilaya na wakurugenzi wa halmashauri hizo kutimiza lengo kabla ya januari,

Hata hivyo amesema kuwa ameanza kupata wasiwasi na utendaji kazi wa Wakuu wa Mikoa hiyo ambayo haijatimiza  mpango wa madawati,kama wataweza kuendana na kasi ya Serikali. 

Video: Mrema alia na jeshi la magereza
MK Dons Kuivurugia Chelsea?