Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ameliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata Mkurugenzi wa zamani wa mamlaka ya vitambulishio vya taifa (NIDA), Dickson Maimu pamoja na wakurugenzi wa kampuni tatu ambazo zinatuhumiwa kujipatia mabilioni ya shilingi toka mamlaka ya vitambulisho vya taifa Nida.

Waziri Lugola ametoa agizo hilo leo Agosti 21, 2018 jijini Dodoma leo baada ya kuzungumza na wakurugenzi wa kampuni tatu za Gotham International Ltd inayodaiwa na serikali zaidi ya bilioni 2.8, Gwiholoto Impex zaidi ya milioni 900 na Aste Insurance broker company ltd inayodaiwa bilioni 1.1 na wakurugenzi wake kukamatwa.

Aidha, waziri Lugola ameagiza kukamatwa kwa baadhi ya watumishi wa mamlaka hiyo ambao walikuwa wakishirikiana na makampuni hayo kujipatia fedha za serikali kinyume na utaratibu.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Agosti 22, 2018
The think tankers of Tanzania yaushukia Ubalozi wa Marekani