Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amepokea michango ya zaidi ya sh. bilioni 1.4 kutoka kwa mabalozi wa nchi za nje nchini Tanzania na Jumuia ya Wafanyabiashara wa Kitanzania kwa ajili ya kusaidia wananchi kufuatia tetemeko la ardhi lilitokea Jumamosi, 10 Septemba, 2016 na  kusababisha vifo vya watu 17 hadi leo na wengine 253 kujeruhiwa. Tetemeko hilo pia limesababisha maelfu ya wananchi kukosa makazi baada ya nyumba 840 kuanguka na nyingine 1,264 zikipata nyufa yakiwemo majengo 44 ya taasisi mbalimbali za umma.

Majaliwa wakati akizungumza katika hafla ya uchangishaji fedha kwa ajili ya kusaidia wahanga hao (Jumanne, 13 Septemba, 2016) amewashukuru kwa michango yao ya fedha na vifaa vya ujenzi ikiwemo mifuko 2,800 ya saruji. Amesema tetemeko hilo ni kubwa na halijawahi kutokea nchini ambapo limesababisha Serikali kuzifunga shule zake mbili za sekondari za Nyakato na Ihungo kati ya nne zilizoathirika vibaya na  tetemeko hilo.

Kesi ya Lema: Mahakama yatoa neno zito Upande wa Serikali
John Terry Kuwakosa Liverpool