Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha kampuni ya SBC Tanzania Ltd kinachotengeneza vinywaji baridi pamoja na kiwanda cha kukata na kung’arisha mawe ya asili cha Marmo Granito Mines Tanzania Ltd, vilivyoko katika eneo la Iyunga Mjini Mbeya.

Majaliwa ametembelea viwanda hivyo kwa lengo la kukagua utekelezaji wa sera ya kujenga uchumi wa viwanda nchini, ambao ndiyo kipaumbe cha Serikali ya Awamu ya Tano.

Akiwa katika kiwanda cha Pepsi, Waziri Mkuu alikagua maendeleo ya ujenzi wa upanuzi wa kiwanda  hicho kwa ajili ya kuanza uzalishaji wa vinywanji baridi kwenye chupa za plastiki, ambapo amewasihi Watanzania kupenda kutumia bidhaa zinazozalishwa kwenye viwanda vya ndani.

Ameishauri kampuni hiyo kuendelea kupanua uwekezaji wake hapa nchini kwa kuwa Tanzania ina sera na mazingira mazuri ya uwekezaji. Kiwanda hicho kilijengwa mwaka 1999 kikiwa na wafanyakazi 75 na kwa sasa kina wafanyakazi 190.

“Nawashauri muendelee kuwekeza Tanzania kwani mbali na utulivu wa kisiasa pia sera na mazingira yake ya uwekezaji ni mazuri.”

 

Kituo kitakachoonesha pambano la Mayweather Vs McGregor
DJ D- Ommy azidi kuwa ‘Wakimataifa’, ashirikiana na DJ Walshy Fire wa Jamaica