Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa Hospitali ya Aga Khan uandae skeli ya mishahara inayofanana kwa watumishi wenye taaluma zinazofafana ili kuondoa manung’uniko baina ya wafanyakazi wa taasisi hiyo.

 

Ameyasema hayo kutokana na malalamiko ya watumishi wa taasisi hiyo ambao wanadai kuwepo kwa tofauti ya mishahara kwa watumishi licha ya kuwa na taaluma moja na kufanyakazi kwenye kituo kimoja.

 

Majaliwa amesema hayo wakati wa ufunguzi wa awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli.

 

Asmeema suala la maslahi kwa watumishi ni muhimu na linatiliwa mkazo na serikali hivyo uongozi wa Hospitali ya Aga Khan fanyeni mapitio ya mishahara hasa kwa watu walio katika taaluma zinazofanana.

 

“Serikali imeunda Tume ya Mishahara na Motisha inayofanya mapitio ya ngazi za mishahara ili kuondoa utofauti wa mishahara kwa watumishi waliosoma ngazi moja, wenye taaluma moja wanaofanyakazi kwenye kituo kimoja.”

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Machi 11, 2019
Ndege ya Ethiopia yaanguka ikiwa na watu 157

Comments

comments