Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeandaa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kwa lengo la kupunguza kiwango cha ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika jamii kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2022.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Novemba 25, 2018 wakati akizindua Kampeni ya siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia katika Uwanja vya Jamhuri jijini Dodoma.

Amesema katika kukabialia na ukatili wa kijinsia Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imekuwa ikichukua hatua mbalimbaliza kuzuia na kutokomeza ukatili.

Majaliwa amesema mpango huo ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia (2000); Mkakati wa Taifa wa Maendeleo ya Jinsia (2005); Sera ya Maendeleo ya Mtoto (2008); Sheria ya Makosa ya Kujamiiana – SOSPA (1998).

Amesema utekelezaji wa mpango huo utachangia katika utekelezaji wa mipango na Mikataba ya Kikanda na Kimataifa kuhusu usawa wa kijinsia, uwezeshaji wanawake na wasichana pamoja na haki na ustawi wa mtoto.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Novemba 26, 2018
Mwanri aainisha maeneo manne ya uwekezaji mkoa wa Tabora

Comments

comments