Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa  alikwenda Gaborone, Botswana kuhudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini  mwa Afrika wa Double Troika ya Asasi ya Siasa Ulinzi na Usalama (SADC Double Troika Summit)  ambao umefanyika leo(Jumanne, Juni 28, 2016). 

Waziri Majaliwa amepata nafasi na kuongea yaliyojiri katika kikao hicho ambapo kubwa ilikuwa ya  Waziri Mkuu wa Lesotho, Dk. Pakalitha Mosisili kukubali kutekeleza masharti yaliyowekwa  (SADC Double Troika Summit), na kuridhia timu ya uchunguzi kwenda nchini humo kufanya uchunguzi wa hali ya kiusalama na kisiasa.

Video: Faulu iliyowamaliza Yanga SC dhidi ya TP Mazembe na 'Highlights' zake (0 - 1)
Tanzania Yagundua Hifadhi Kubwa Yenye Gesi Adimu, Rasilimali Zinawasaidiaje Watanzania?