Waziri wa Katiba na Sheria, Harrison Mwakyembe ameshindwa kuzuia hisia zake Bungeni Dodoma wakati akitoa sala za kuaga mwili wa Spika mstaafu, Samuel Sitta. Amesema kifo cha mzee Sitta ni pigo kubwa sana kwake, kwa wapigania haki wote na Taifa kwa ujumla hivyo ameuombea mwili wake upumzike kwa amani na daima Taifa litamkumbuka kwa ushujaa wake.

Mwili wa Samuel Sitta umefikishwa Bungeni Dodoma ili kupata heshima za mwisho kutoka kwa wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, viongozi wa mkoa pamoja na wananchi wengine. Kabla ya kufikishwa Bungeni mwili wa mzee Sitta uliagwa Dar es salaam ambapo Rais John Pombe Magufuli aliongoza viongozi wengine na wananchi kuaga mwili huo katika viwanja vya Karimjee kisha kuelekea Dodoma.

Mzee Samuel John Sitta alifariki dunia Novemba 7, 2016 katika Hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani

Video: Wabunge walivyopokea mwili wa Samuel Sitta Bungeni Dodoma

Janeth Magufuli aruhusiwa kutoka hospitalini
Majaliwa aongoza Wabunge kuaga mwili wa mbunge Hafidh Ally