Muigizaji Wema Sepetu amekutana na swali la mwandishi wa habari aliyemtaka kumpa ushauri Zari ambaye ni mama watoto wa aliyekuwa mpenzi wake, Diamond Platinumz.

Wakati wadau wa burudani wakiwa na kumbukumbu ya maelezo ya Zari kuwa kitendo cha Diamond kumshika Wema hadharani ni moja kati ya sababu za kuachana naye, Wema amesema hawezi kuwa mshauri wake.

“Mimi siwezi kuwa mshauri wa Zari, hapana…” alisema Wema na kuanza kuhepa vikuza sauti vya waandishi wa habari vilivyokuwa vimemzunguka akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Katika hatua nyingine, Wema alisisitiza kuwa hana uhusiano wa mapenzi na Diamond na kwamba hivi sasa atakuwa Bosi wake kwani mrembo huyo atakuwa na kipindi ‘Wafasi TV’.

Wema alijitetea kuwa alialikwa kwenye hafla ya WCB kama rafiki na hakuna kitu cha kimapenzi alichofanya na Diamond siku hiyo kwani kukumbatiana ni kawaida, “Me and Diamond didn’t kiss… I got nothing to do with Diamond, right now.”

Amedai huenda Zari alikuwa na sababu nyingine za kufikia uamuzi wake lakini sababu aliyoitoa kuhusu tukio la Wema na Diamond haliwezi kuwa sababu ya kweli.

Angalia video hapa kuona mahojiano yote:

Township Rollers: Tunaifahamu vizuri Yanga
Hali ya Mbowe kiafya yatetema, akimbizwa KCMC

Comments

comments